Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva .
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa inaongeza muda wa siku
nne tu wa kuandikisha wapiga kura kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.
Hii inamaanisha kuwa zoezi hilo ambalo lilikuwa linaisha ijumaa ya kesho
julai 31, litaendelea hadi jumanne agosti 4Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa hataweza kuongeza muda wa zaidi ya siku nne kwa kuwa ratiba zitaingiliana.
Aidha, Jaji Mstaafu Lubuva amesema mpaka sasa watu zaidi ya milioni
18 wameandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa njia ya
mfumo wa kielektroniki BVR kwa nchi nzima.

Note: Only a member of this blog may post a comment.