JOTO YA JIWE! MRAMBA, YONA WAKESHA WAKILIA GEREZANI!
Mramba
(kushoto) akiteta jambo na wakili wake, Peter Swai baada ya Mahakama
kumhukumu miaka mitatu jela na faini ya shilingi milioni tano.
Harun sanchawa na denis mtima JOTO
ya jiwe! Wafungwa wawili wapya katika gereza la Ukonga jijini Dar es
Salaam, Waziri wa zamani wa Fedha, Basil Mramba na mwenzake wa Nishati
na Madini, Daniel Yona, wanadaiwa kukesha huku wakilia katika siku
wakianza kutumikia kifungo chao cha miaka mitatu baada ya kukutwa na
hatia ya matumizi mabaya ya ofisi, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa
Kisutu jijini Dar es Salaa Jumatatu iliyopita.
Kutoka kushoto ni Basil Mramba, Daniel Yona na Gray Mgonja wakiteta jambo.
Basil Mramba akionekana ndani ya defenda la Polisi kuelekea Gereza la Ukonga jijini Dar.
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona (katikati) akitoka katika chumba cha Mahabusu baada ya hukumu hiyo kutolewa.
Kwa mujibu wa chanzo chetu ndani ya gareza hilo, Mramba na Yona,
ambao walikuwa mawaziri katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa awamu tofauti, waliohukumiwa kifungo hicho na Jaji wa
Mahakama Kuu, Sam Rumanyika katika kesi iliyochukua zaidi ya miaka nane
tokea walipopandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza, wakiwa na aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Nishati, Agrey Mgonja, muda mwingi walionekana watu wenye
mawazo huku wakijifuta machozi machoni mwao.
Baadhi
ya ndugu na jamaa wa Basil Mramba na Daniel Yona wakiondoka katika
Mahakama ya Kisutu kwa masikitiko makubwa baada ya kupelekwa gerezani.
“Nadhani hawakutegemea kama kweli watafika hapa, maana walionekana
wenye huzuni sana. Lakini wakati wao wakiwa katika hali hiyo, wafungwa
wengine walikuwa wakishangilia kwa sababu ni jambo geni kwao kuwaona
vigogo gerezani, hasa waliowahi kushika nyadhifa kubwa kama zao. Hali
siyo nzuri kwa kweli,” kilisema chanzo hicho.
Aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Gray Mgonja (katikati)
akionekana mwenye furaha baada ya kuachiwa huru na Mahakama.
Katika kesi yao, mawaziri hao waandamizi walituhumiwa pamoja na mambo
mengine, kutumia vibaya madaraka yao yaliyosababisha hasara ya shilingi
bilioni 11 kwa serikali.
Lango kuu la Mahakama ya Kisutu kabla ya kuondoka defender la Polisi.
Hawa wanakuwa viongozi wa kwanza waliowahi kufikia ngazi ya uwaziri
kuhukumiwa jela tokea kuondoka kwa Rais wa Kwanza wa Tanzania, Hayati
Mwalimu Julius Nyerere ambaye serikali yake ilimfunga aliyepata kuwa
waziri Abdalah Fundikira (sasa aliyepata marehemu).
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Note: Only a member of this blog may post a comment.