Gladness Mallya na Gabriel Ng’osha BAADA
ya vuta nikuvute ya wazazi wa wanafunzi, Hilary na Hamis ‘watoto wa
Diamond’ walioshinda katika shindano la kucheza Ngololo mwaka jana na
staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuahidi kuwasomesha
katika shule ya East Africa International iliyopo Mikocheni, Dar huku
akishindwa kuwalipia ada na watoto hao kurudishwa nyumbani, hatimaye
wamerejeshwa tena shuleni.
Ilidaiwa kwamba wamewakataza kuzungumza kwenye vyombo vya habari
kutokana na kwamba walichukizwa na habari hiyo kuvuja na kuripotiwa na
gazeti hili kwa mara ya kwanza.
“Wale watoto wamerudi shule tayari baada ya kukaa nyumbani kwa miezi
kadhaa, naamini hata gazeti lenu lilisaidia sana kuwashtua kwani
vinginevyo wasingerudi na ndiyo maana hata wazazi waliambiwa wasiongee
na ninyi,” kilisema chanzo hicho.
Naye mmoja wa wazazi wa watoto hao kwa sharti la kutokutajwa alisema:
“Kwa sasa niko safarini ila ni kweli watoto wamerudi shule ila mambo
bado hayajawa mazuri sana, sema ndiyo wako kwenye mazungumzo zaidi na
suala hilo nimewakabidhi ndugu zangu ambao wako eneo la tukio ili
walishughulikie.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.