Thursday, July 9, 2015

Anonymous

ISABELLA: NIMENASA TENA!

Isabella Mpanda ‘Bella’
Na Brighton Masalu
‘MCHUNGULIAJI’ katika anga la muziki na filamu, Isabella Mpanda ‘Bella’ amekiri kushika ujauzito huku akimtaja mwenye ‘mzigo’ huo kuwa mpenzi wake wa sasa, Luteni Karama.
‘Akishushuana’ kwa sauti za kukwaruza na Amani huku akibugia udongo mwekundu (pemba) Ijumaa ya wiki iliyopita katika nyumba anayoishi Kijotonyama jijini Dar, msanii huyo alisema haoni tabu kupata ujauzito na mtu anayempenda na kwamba fahari ya mwanamke ni kuzaa na amejiandaa kwa majukumu ya kulea mimba na watoto. 

Hata hivyo, mwandishi wetu alimuuliza juu ya umri wa mimba lakini aligoma kutaja na kushikilia kile alichokiita mimba yake siyo matangazo kisha akaendelea kubugia udongo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.