VUNJA ukimya! Mfalme wa Bongo
Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kwa mara ya kwanza amefunguka
kuhusiana na sakata la watoto alioahidi kuwasomesha kushindwa kuendelea
na masomo kwa sababu ya ada.
Diamond alifunguka kuwa kutokana na
kumwamini mtu huyo na yeye kuwa ‘bize’, alishindwa kupata muda wa
kufuatilia kwa ukaribu sakata hilo hadi aliposhtushwa na habari
iliyoripotiwa na gazeti hili.
“Nilisiktishwa sana, nilitoa fedha zote,
nikampa mtu ambaye nilimuamini sana lakini kwa tamaa zake akaamua
kuzitumia fedha hizo, unajua muda wangu ni mchache sana, hivyo
sikufuatilia, lakini kwa sasa mambo yote yamekaa sawa,” alisema Diamond.

Note: Only a member of this blog may post a comment.