Msanii mwingine wa Tanzania, Lady Jaydee ameongezeka kwenye orodha ya
wasanii wa Tanzania ambao video zao zimeingia kwenye chart za vituo
vikubwa vya TV vya kimataifa.
Wiki iliyopita baada ya video ya Joh Makini ‘Nusu Nusu’ kushika namba
1 kwenye chart ya video za wasanii wa Afrika ya MTV Base, na Diamond
kukamata nafasi ya kwanza kwenye chart ya Trace Urban, mwanamuziki wa
kike Lady Jay Dee pia ameingia kwenye orodha hiyo.
Video ya Jide ‘Give Me Love’ aliyowashirikisha wasanii wa Afrika
Kusini, Uhuru, Mazet na Maphorisa, imeingia na kukamata nafasi ya 5
kwenye Official African Chart ya MTV Base wiki hii, huku Joh Makini
akishuka kwa nafasi moja hadi nafasi ya pili.

Note: Only a member of this blog may post a comment.