Diamond Platnumz amesema kuwa yuko tayari kufanya collabo na msanii yeyote wa Tanzania, ambaye atakuwa anakidhi vigezo vyake.
Muimbaji huyo wa ‘Nana’ ameyasema hayo baada ya kuulizwa kwanini hafanyi collabo nyingi na wasanii wa Tanzania.
“Mimi sina tatizo as long as nijue hiyo kazi unayotaka kufanya na mimi itafika wapi,” alisema Diamond kupitia Clouds FM.
“umejipanga vipi project yako na umeiandaa vipi, kwasababu sitaki
nifanye tu nyimbo mwisho wa siku halafu iishie tu ndani unaiskiliza
wakati natumia muda kukaa kuandika kupoteza muda studio.“
Aliendelea kwa kujitolea mfano yeye anapofanya collabo na msanii wa
nje, lengo kubwa huwa ni kujitangaza zaidi kule anakotoka msanii
anayemshirikisha.
“Na ukiangalia kwa mfano kama nje nakuwa nafanya collabo na
wasanii tofauti tofauti kwasababu inasaidia pia muziki wetu kutanua
kiurahisi[…] Lakini haimaanishi kwamba sitaki kufanya collabo na wasanii
wa Tanzania […] yaani unavyokuja kufanya collabo lazima ufanye kuonesha
qualification za kufanya tufanye collabo.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.