MKURUGENZI wa kampuni ya Bench Mark Production, Rita Poulsen (Madam
Rita) jana, Jumanne, alitayarisha futari kwa watoto yatima wa kituo cha
Chakuwama kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam ikiwa ni harakati za
kuanza mchakamchaka wa shindano la Bongo Star Search (BSS) la kutafuta
vipaji vya uimbaji ambalo linatarajiwa kuanza Julai 4, jijini Mwanza.
Katika hafla hiyo, Rita aliongozana na jaji mwenzake wa muziki,
Master J,Rita alisema ameamua kutembelea kituo hicho ili kurejesha
fadhila zake kwa jamii kwa kile kidogo anachokipata.
“Nimeamua kuwafuturisha watoto hawa ukiwa mkakati wa kutembelea vituo
mbalimbali ili kurejesha fadhila yangu kwa jamii.“ Tumeamua kufanya
mabadiliko makubwa katika shindano la mwaka huu na nina imani kila kitu
kitakwenda sawa,” alisema Rita.

Note: Only a member of this blog may post a comment.