Maofisa wa usalama barabarani wakichukua taarifa eneo la ajali.
Coaster baada ya kuigonga treni.
Wananchi wakishuhudia ajali hiyo.
WATU watano wamepoteza maisha huku 24
wakijeruhiwa baada ya basi la abiria kuligonga treni lililokuwa linatoka
Morogoro – Dodoma leo Jumatano asubuhi katika eneo la Kibaoni, wilayani Kilosa
mkoani Morogoro. Basi lililohusika katika ajali hiyo ni aina ya Isuzu Coaster lenye namba za usajili T837 CTM linalomilikiwa na Feisal A. Khuwel wa wilayani Kilosa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa ajali hiyo imetokea leo (Jumatano) majira ya saa 1 asubuhi na imetokana na uzembe wa dereva wa basi.
Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wiaya Kilosa, Dickson Masale amethibitisha kupokea miili ya watu watano akiwemo dereva wa basi pamoja na majeruhi 24.

Note: Only a member of this blog may post a comment.