Brighton Masalu
VUNJA ukimya!
Baada ya kuhusishwa kwa muda mrefu na fununu za kutembea na wanaume
kadhaa tangu kufariki kwa aliyekuwa mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’,
msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma hatimaye amefunguka na kujiapiza
kwa kulamba kidole, kuchovya mchanga na kukipitisha shingoni akidai
tangu kuondoka kwa Sajuki hajawahi ‘kuchangia shuka’ na mwanaume yeyote
na kama yupo, ajitokeze hadharani!
“Nashangazwa sana na wanaoeneza uvumi wa mimi kutembea na wanaume wengi baada ya kifo cha mume wangu, kwani mimi sina haki kama mwanamke jamani? Kama kuna mwanaume mwenye uthibitisho wa kutembea na mimi si ajitokeze!” alisema Wastara huku akiashiria jazba.

Note: Only a member of this blog may post a comment.