Friday, June 5, 2015

Anonymous

Mtoto wa MONALISA Alishangaa Siku ya Msiba wa Baba Yake!

Marehemu George Tyson enzi za uhai wake akiwa na mtoto wake Sonia
Sonia Tyson George mtoto wa aliekuwa muongozaji mkubwa wa fialamu hapa , Marehemu George Tyson amesema kuwa siku ya msiba wa baba yake alishangaa sana kuona watu wengi nyumbani kwao na kuamini kuwa baba yake ni mtu maarufu katika jamii.

Ikiwa ni mwaka mmoja sasa umepita tangu baba yake afariki dunia, Sonia akiongea kwenye kipindi cha filamunata alisema kuwa mbali na baba yake ni kitendo ambacho hatokisahu katika maisha yake lakini anajikaza na kujipa moyo kwa sababu ni kazi ya Mungu

“Ilikuwa ni tabu kuami kuwa nimefiwa na baba lakini ndo basi imeshatokea sina la kufanya namuachia Mungu kwa hili lililobaki ni muombea apumzika kwa amani tu kwani nimemisi vitu vingi kutoka kwake hasa kunidekeza kwake “ alisema Sonia

Marehemu George Tyson ameacha pengo kubwa takika tasnia ya filamu nchini ambapo alikuwa mwongozaji wa filamu ya Girl Friend iliyoleta mapinduuzi makubwa mpaka sasa katika soko zima la filamu

Pia George Tyson amewatoa mastaa wakubwa ambao sasa wanamiliki vipindi vyao wenyewe kama Joyce Kiria wa Wanawake Live na Mboni Masimba wa the Mboni Show.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.