Wednesday, June 24, 2015

Anonymous

TAMBWE: Nitavaa jezi ya NGASSA!


ssdStraika wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe.
Ibrahim Mussa, Dar es Salaam
WAKATI mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Mrisho Ngassa, akitoa onyo kwa mchezaji atakayetaka kuivaa jezi yake namba 17, straika wa timu hiyo, Mrundi, Amissi Tambwe, ameweka wazi msimamo wake juu ya jezi hiyo, akisisitiza lazima ataivaa msimu ujao.
beki+msimbaziJezi namba 17 ya mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Mrisho Ngassa.
Tambwe aliwahi kuiomba jezi hiyo iliyokuwa ikitumiwa na Ngassa mara baada ya kutua Yanga akitokea Simba, lakini ilishindikana kwa kuwa tayari alikuta inatumika ndani ya kikosi hicho kabla ya kuamua kuitumia jezi namba 19.

Akizungumza na Championi Jumatano, Tambwe alisema kuwa kamwe hawezi kuogopa onyo hilo na kuiacha jezi hiyo kwa kuwa ndiyo jezi anayoipenda zaidi tangu alipotua Tanzania na sasa anaamini ni haki yake kuivaa kwa kuwa Ngassa tayari ameshaondoka na kujiunga na Klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini.

“Unajua wakati najiunga Yanga niliomba hiyo jezi, lakini haikuwezekana kwa sababu tayari ilikuwa inavaliwa na Ngassa, ikanibidi nichukue namba 19 sasa kwa kuwa ameondoka basi nitaivaa kwa sababu ndiyo jezi ninayoipenda.

“Hakuna kitakachonifanya niogope, maana Ngassa kwa sasa siyo mchezaji wa Yanga na wala siwezi kumuomba aniruhusu. Inajulikana dunia nzima kuwa mchezaji akiondoka jezi hupewa mtu mwingine. Naamini lazima niichukue kwani hata Simba nilikuwa navaa jezi hiyo,” alisema Tambwe.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.