Thursday, June 4, 2015

Anonymous

Soudy Brown yuko na Diamond, Wema na Linah.. Ishu ni picha inayowaonesha Wema na mpenzi wa zamani wa Linah !!

PhotoGrid_1433422565118
Soudy kainasa story kwamba kuna picha inayowaonesha Wema Sepetu na Naga, ambaye alikuwa mpenzi wa Linah.. Kuna uhusiano wowote unaendelea kati yao hii??
Hapa akaanza na Linah.. yeye kasema uhusiano wake na Naga uliisha zaidi ya miezi miwili iliyopita kwa hiyo kaendelea na maisha yake hajui kama kuna uhusiano unaoendelea kati ya Wema na Naga. 

Akamcheki Wema ambae alikataa kuongea chochote; “Soudy sijisikii kuongea siko kwenye mood“>> Wema Sepetu.
Mwisho Soudy akamcheki Diamond Platnumz, jamaa akasema hamjui huyo aliyekuwa mpenzi wa Linah na hakuwahi kuwa na uhusiano na Linah kwa vile ni kama mdogo wake.
U Heard iko kwenye hii sauti, bonyeza play hapo chini utamsikia Soudy anavyoongea na wote watatu...
-via millardayo

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.