Thursday, June 4, 2015

Anonymous

HABARI PICHAZ: Baada ya ajali ya lori la mafuta Nigeria, hii nyingine ni kituo cha mafuta kuwaka moto Ghana


Mapema wiki hii  tuliandika stori ya ajali ya lori la mafuta kuua zaidi ya watu 90 Nigeria ikiwa ni baada ya kuwa kwenye mwendo mkali na kugonga watu na magari yaliyokuwa kwenye kituo cha abiria.

Muonekano wa kituo cha mafuta baada ya kulipuka
Lakini leo Ghana nayo imeingia kwenye headlines baada ya kituo cha mafuta kulipuka na kuua watu wanaokadiriwa kuzidi 90 katika mji mkuu wa nchi hiyo Accra.

Mlipuko huo umetokea baada ya mvua kubwa iliyosababisha mafuriko katika maeneo mengi ya mji huo ambapo pia imewaacha watu wengi bila makazi huku sehemu kubwa ya mji ikiwa gizani kutokana na kukatika kwa umeme.

Mwili wa mtoto ukiokotwa katika eneo la kituo hicho
Idadi ya watu waliofariki huenda ikaongezeka kwani watu wengi wamepoteza maisha baada ya kuwepo kituoni hapo wakijikinga na mafuriko yaliyotokea na huenda idadi ikaongezeka kutokana na baadhi ya miili kuwa bado haijapatikana.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.