Saturday, June 20, 2015

Anonymous

MTIBWA SUGAR yawabeba Baba UBAYA, BAHANUZI bila kinyongo!

Martha Mboma, Dar es Salaam 
MTIBWA Sugar wala haina kinyongo na sasa ipo katika mchakato wa kuwarejesha wachezaji wake walioachwa na Simba na Yanga ili waanze upya harakati zao za soka.

Muda wowote kuanzia sasa Mtibwa ya Turiani, Morogoro itakuwa imeshawarejesha beki wa kushoto Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ kutoka Simba na straika Said Bahanuzi kutoka Yanga. Pia imepanga kumsajili Haruna Chanongo aliyemaliza mkataba Simba.

Kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya klabu hiyo, wachezaji hao wameshafanya mazungumzo ya awali na klabu hiyo na muda wowote kuanzia sasa watasaini mikataba yao.

“Wala hatuna matatizo na hao wachezaji kwani waliondoka kwa heshima na tunawarejesha baada ya mambo yao kukwama, tutahakikisha tunamalizana nao muda wowote na hata huyo Chanongo tutamsajili,” kilisema chanzo.

Alipotafutwa Ofisa Habari wa Mtibwa, Thobias Kifaru alisema; “Kwa sasa hatujafanya usajili wowote, zaidi tunasubiri bodi ya timu ikutane kujadiliana ishu ya usajili na mambo ya kocha.” Mtibwa ipo katika mchakato wa kumpa kazi Kocha Piet De Mol kutoka Ubelgiji kuchukua nafasi ya Mecky Maxime ambaye tayari ameanza kazi Taifa Stars kama kocha msaidizi.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.