Saturday, June 20, 2015

Anonymous

BARTHEZ: Mashuti ya Mwashiuya hatari nyie!

Ibrahim Mussa, Dar es Salaam
MASHUTI ya kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga, Geofrey Mwashiuya ni hatari hasa akiupatia mpira na kulenga lango ipasavyo, ukibisha muulize kipa Ally Mustapha ‘Barthez’.

Barthez aliliambia Championi Jumamosi kuwa, kwa siku chache alizofanya mazoezi na Mwashiuya anayemudu kucheza winga ya kushoto, amebaini dogo huyo ni hatari sana kwa kupiga mashuti.

Mwashiuya ambaye amejiunga na timu hiyo hivi karibuni akitokea Kimondo FC ya Daraja la Kwanza yenye makao makuu yake jijini Mbeya amekuwa mwiba mchungu kwa Barthez kutokana na uhodari wake wa kupiga mashuti makali hata anapokuwa nje ya eneo la hatari. Barthez alisema: “Huyu dogo anapiga mashuti makali sana ambayo kama ukikosea kidogo tu katika harakati za kuzuia unaweza kuumia kwani huwa anapiga kwa nguvu sana hasa akiwa mbali.”“Namuomba asipunguze kasi hiyo, anatakiwa kuiongeza zaidi ya hapo kwa faida yake mwenyewe na klabu.”

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.