Christian Bella ni muimbaji anayeamini kuwa ili msanii afanikiwe zaidi anahitaji kuwa na management nzuri.
Muimbaji huyo wa ‘Nashindwa’ ameisifia management ya Diamond na kuongeza kuwa endapo angeweza kuwa na watu imara wa kumsimamia angekuwa mbali zaidi ya hapo alipo.
Muimbaji huyo wa ‘Nashindwa’ ameisifia management ya Diamond na kuongeza kuwa endapo angeweza kuwa na watu imara wa kumsimamia angekuwa mbali zaidi ya hapo alipo.
- “Mi napenda kusema ukweli, Diamond yuko vizuri na management yake wanajitahidi vizuri, yeye msanii akiwa na management nzuri yaani Babu Tale na Fella nawapa bigup sana.”Alisema Bella kupitia 255 ya Clouds Fm. “Ndo tunataka watu kama wale wawepo, mimi nikipata watu kama wale wee! itakuwa mbali sana kwasababu mimi najua kwamba mimi ninauwezo wa kuimba nina vocal najua melody za kuimba, ila nakosa tu watu wa kukunyanyua, kwamba lala usingizi tunaenda kuongea na Fally Ipupa, we lala yaani zima simu wanakwambia we studio kesho, aah yaani naenda nauwa, ndo wasanii wa mbele wanaishi hivyo.” alimaliza.


Note: Only a member of this blog may post a comment.