Jeshi la Polisi Dar limebaini mabaki ya mwili wa mmiliki wa shule ya Mtakatifu Zion, Anna Mizinga aliyeuawa Desemba mwaka jana na kutupwa kwenye shimo la choo cha shule yake.
Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova
alisema mabaki ya mwili huo yalibainika Juni mwaka huu na tayari watu
watatu wanashikiliwa na Polisi wakidaiwa kufanya unyama huo.
Akifafanua juu ya tukio hilo Kova
alisema Februari mwaka huu mtu mmoja alitoa taarifa polisi juu ya
kupotea kwa mmiliki huyo tangu Desemba mwaka jana saa 11 jioni na
hakuonekana tena.
Alisema mmiliki huyo alindoka nyumbani
kwake na gari dogo aina ya Verosa akiwa na mtu mmoja ambaye naye ni
miongoni mwa watuhumiwa wanaoshikiwa na jeshi hilo na abada ya taarifa
hiyo walifungua jalada la uchunguzi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa
hao.
Alisema mtuhumiwa wa kwanza alikamatwa Uchira, Moshi na kuwataja wenzake.
“Katika
mahojiano mmoja alisema yeye na marehemu waliondoka hadi shuleni kwake
na walipofika walivamiwa na watu wapatao wanne na kuanza kupigwa, lakini
yeye alifanikiwa kutoroka na kujificha katika uzio wa shule, na
aliwaona watu hao wakiendelea kumpiga mama huyo na kisha kumtupa katika shimo la choo kisha kutokomea na gari lake kusikojulika” Kova.
Watuhumiwa hao wanaendele kuhojiwa ili
kupata undani wa tukio hilo, ikiwa ni pamoja na kuwatafuta na kuwakamata
watuhumiwa wengine wanaohusika na tukio hilo.


Note: Only a member of this blog may post a comment.