Leo kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii mwanadada Amanda Poshy amezua maswali yasiyo na majibu baada ya kuandika maneno ambayo wengi wameshindwa kujua yana maana gani kwani yamekaa kimafumbo flani hivi.
Kauli hii ya mwanadada Amanda inakuja siku chache tu baada ya mrembo Irene uwoya kuongelea jambo kama hili hili siku mbili zilizopita.
Amanda poshy ameongelea mambo mengi yakiwemo “Kuchukuliana mabwana kwa waigizaji wa kike”, “unafiki”, “kusemana vibaya kwa wasanii” wa kike na mengine mengi kitu kilichofanya wengi washindwe kujua ni lipi hasa limemkumba mwanadada huyu aliyejaliwa umbo namba 8.
Hichi ndicho alichosema mwanadada Amanda poshy.
“…Dunia ina mambo mengi Sana...Dunia hii ina watu Wa kila aina....binaadam tunachekeana lakini wengi tuna roho za kishetani..Wasanii hatupendani,wasanii siye siye kutwa kuchukuliana mabwana,wasanii siye siye kutwa kusemana vby,wasanii siye siye kutwa kufanyiana unafki na unyama Wa chini kwa chini...tunachekeana kichina China ila hakuna kitu kikubwa na kizuri cha kumshukuru Mungu endapo atakuonyesha mnafki wako namba moja...sijazoea vya haramu kama wewe na ndio maana niliridhika na kile kidogo nilichotaka kukipata...Sintokutaja wakubwa wangu wamenizuia ila unajijua na umejiumbua mwenyewe ila nakuambia hapa hadharani my dia huwa sipendi kuongea ...huwa sipendi maneno ila umefanikiwa hilo basi subiri na lingine “coz” hapa siyo mwisho lakini jua kuwa unafki na ubaya wako hautokufikisha popote utaishia hivyo hivyo labda Kama Mungu mjomba wako lakini Kama ni Mungu wetu sote wacha tuone mwisho wake..wacha mie niendelee kutafuta kile kidogo na wewe endelea kufanya unafki wako....Kitu kimoja tambua HUJANIKOMOA NA HAUTONIKOMOA KAMWE......”
Wachunguzi wa mambo wanadadisi kuwa itakuwa ni lile jambo la kwanza kabisa tulilolitaja hapo juu!
Hatari sana bongo movies!

Note: Only a member of this blog may post a comment.