Wednesday, May 13, 2015

Anonymous

VIDEO: LULU Michael Kuimba Muziki Wa Injili!

Lulu aliweka wazi kupitia The Sporah Show kuwa kama ikitokea siku akawa mwimbaji basi anachagua kuimba muziki wa injili.
“Napenda kuimba na nadhani naweza kuimba, napenda kama siku itatokea nimekuwa mwimbaji niimbe gospel, napenda sana gospel.”

Alipoulizwa kuhusiana na uhusiano wa maisha yake ya nje na imani yake hiki ndicho alijibu.
“Yaani vimini vyote whatever it is lakini kiukweli I‘m God fearing yaani namwogopa sana namheshimu sana Mungu, sio kumwogopa peke yake. Kwahiyo pamoja na yote ninayoyafanya imani yangu iko pale pale hata Mungu anajua. Mnanijua kwa nje, huo ndio upande mnaoujua, kuna upande wangu wa ndani, na hamuwezi kuujua lazima muwe watu wa ndani sio kila mmoja anaweza kuujua.”

Lulu aliwahi kuthibitisha kuwa anaweza kuimba, alipopanda jukwaani na kuimba live na bendi wimbo wa Lady Jaydee ‘Yahaya’ kwenye uzinduzi wa filamu yake ‘Foolish Age’ mwaka juzi (2013).
Kama hukuwahi iona video hiyo icheki hapa chini...

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.