Wednesday, May 13, 2015

Anonymous

MSIBA: Enock Bella wa Yamoto Band afiwa na mama yake mzazi, alikuwa akijifungua huko Zanzibar!

Msanii wa kundi la Yamoto Band, Enock Bella amefiwa na mama yake mzazi. Kwa mujibu wa Said Fella Mama Bella amefariki akiwa Zanzibar wakati akijifungua hospitali.
“Awa wanangu wa family ya mkubwa na wanawe NI ndugu wa kuzaliwa tumbo moja muu na enock bella msanii wa ya moto band jana USIKU wamefiwa na mama mzazi jana alipokuwa akijifungua hospital mjini zanzibar mpango wa mazishi yanafanyika mda huu znz chwaka .R.I.P MAMA. MUNGU AKUWEKE SEHEMU STAHIKI INSHAALLAH,” ameandika Fella kwenye picha hiyo juu aliyoiweka Instagram.

“Pia nawasii wanangu muu na enock bella kifo NI daraja la ibada ya kwenda maisha mengine na kila mmoja wetu anatakiwa kuvuka ila kweli umri wenu mdogo kulibeba ili ila INSHAALLAH MUNGU atawaongezea SUBRA amin lab la aminiiii,” ameongeza Fella.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.