Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kinaweza kujikaanga kwa mafuta yake, iwapo kitachelewa kutangaza
mgombea urais katika kinyang’anyiro cha Uchaguzi mkuu wa Oktoba 25,
mwaka huu.
Sumaye alisema hayo baada ya kuombwa na
waandishi wa habari mjini hapa, wakimtaka azungumzie hali ya kisasa
nchini, uchaguzi mkuu ndani ya CCM na hali ya utekelezaji wa adhabu ya
kifo dhidi ya watu waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa.
Alisema wengi wana shauku ya kufahamu
atakayepeperusha bendera ya CCM kugombea urais, hiyo ikiwa ni kutokana
na kupewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo, na kwamba katika hali
isiyo ya kawaida kimechelewa kumtaja.
“Anapotangazwa
mapema watu wanatafiti, kufahamu ubora wake na kuwa na msimamo wa
kumchagua, hata mgombea anapata muda wa kutosha kufikiri na kufanya
kampeni za kutosha,” alieleza.
Alisema pia hiyo itasaidia wapinzani
kukosa muda wa kutosha kumshambulia mgombea anapotangazwa kwa kuchelewa,
hata yeye mgombea anaathiriwa kwa kutopata muda wa kutosha kufanya
kampeni.
Wananchi nao hawapati muda wa kutosha
kutafiti ili kufahamu ubora wake, ikiwa ni pamoja na kumhoji maswali,
ili wasifanye uchaguzi kwa kufuata mkumbo.
“Hata
mimi hali hii sijaielewa, katika hali ya kawaida sasa hivi wenye nia ya
kugombea wangeshachukua fomu na kuingia mikoani kutafuta wadhamini, kwa
mfano, uchaguzi wa mwaka 2005, mgombea alitangazwa Mei 05,” Sumaye,
Sumaye alisema anaamini siku siyo nyingi
ratiba ya wenye nia ya kuwakilisha chama katika kugombea urais, ubunge
na udiwani itatolewa na chama hicho.
Note: Only a member of this blog may post a comment.