
Hawa Kundani (mwenye vazi jeusi), anayedai kuzaa na kutelekelezwa na mbunge wa Dimani, Abdallah Sharia Ameir, akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kuvamia kikao cha Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kilichokuwa kikifanyika Dar es Salaam siku zilizopita.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuamuru Mbunge wa Jimbo la Dimani Zanzibar, Abdallah Sharia Ameir (CCM)
kutoa Sh 200,000 kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya mtoto wake wa
kiume, mwenye umri wa miaka mitatu na nusu, anayedaiwa kumtelekeza.
Pamoja na amri hiyo, Hakimu Mkazi, Hellen Liwa
alisema mbunge huyo atatoa kiasi hicho cha fedha kuanzia siku alipokoma
kutoa matunzo na matibabu kwa mtoto huyo, anayetajwa kuwa ni mlemavu.
Pia, aliamuru mtoto huyo kulelewa na
wazazi wake na siyo bibi yake, kama alivyokuwa akitaka mbunge huyo.
Hivyo ataendelea kukaa na mama yake.
Kwa upande wake, Wakili Gideon Mandes aliyekuwa akimtetea Hawa Deus aliyekuwa mke wa mbunge huyo, alisema kupitia hukumu hiyo Mahakama imetoa uamuzi wa haki.
“Kupitia
hukumu hii nimebaini wazazi wanawajibu wa kumtunza mtoto wanayemzaa
bila ya kujali hali yake hata kama ni ya ulemavu asitelekezwe na
imedhihirisha hakuna mtu aliye juu ya sheria na kwamba sheria ipo sawa
kwa kila mtu,”.
Wakili huyo aliwashauri Watanzania wenye
matatizo na changamoto kama hizo, kuweka bidii ya kuijua sheria na
taratibu zake ili waweze kuitumia kupata haki na suluhisho kupitia
Mahakama.
Note: Only a member of this blog may post a comment.