Miezi michache baada ya kuuzindua mtandao wake wa Tidal, Jay Z ameanza kupata pigo.
Bloomberg Businessweek imeripoti kuwa label ya Sony inataka kutolewa
kwa nyimbo zake zote kwenye mtandao huo, zikiwemo za mke wake Beyonce
ambaye pia ni mmiliki mwenza wa mtandao huo.
Kwa mujibu wa vyanzo, Jay Z bado hajakamilisha makubaliano ya mkataba
na Sony ambao wanataka walipwe kiasi kikubwa cha fedha kama kianzio
kwaajili ya kutoa haki za kuwekwa kwa nyimbo zao.
Universal na Warner tayari wameshamaliza makubaliano na Tidal.
Kama Jay Z atashindwa kuwalipa Sony fedha wanayoitaka, Bloomberg
imesema nyimbo za wasanii wake wengine wakiwemo Daft Punk, Alicia Keys,
na Usher zitaondolewa kwenye Tidal.
Hivi karibuni Sony ilifuta nyimbo zake kutoka kwenye mtandao wa
SoundCloud kwa sababu hizo hizo. Hata hivyo Bloomberg imedai kuwa Tidal
iko vizuri kifedha na hivyo hili linaweza kuwa ni suala dogo.
-via bongo5
Note: Only a member of this blog may post a comment.