Friday, May 15, 2015

Anonymous

MSIBA: MWANAMUZIKI MFALME WA BLUES, BB KING AFARIKI DUNIA AKIWA USINGIZINI!


 Riley B. King 'BB King'.
MFALME wa Blues, mpiga gitaa na mwimbaji, Riley B. King 'BB King' wa nchini Marekani amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 89 akiwa usingizini huko Las Vegas jana.

King alifahamika kwa baadhi ya nyimbo zake kali kama My Lucille, Sweet Little Angel na Rock Me Baby.
Marehemu alizaliwa Mississippi na kuanza kutumbuiza miaka ya 1940.

Miezi ya nyuma marehemu alikuwa na matatizo ya kiafya na hivi karibuni alipelekwa hospitali akisumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.