Khadija Mngwai,Dar es Salaam
WENGI wanaamini Deus Kaseke aliyesajiliwa na Yanga kwa dau la Sh Milioni 35 ndiye mbadala wa kiungo mshambuliaji Mrisho Ngassa aliyejiunga na Free State Stars ya Afrika Kusini, kumbe siyo kabisa.
Kwa kauli yake, Kaseke anayemudu kucheza winga ya kushoto alisema ni vigumu kwake kucheza kama Ngassa kwani ana vitu vingi anavyozidiwa na mchezaji huyo lakini atajitahidi kumfikia.Akizungumza na Championi Jumamosi, Kaseke alisema Ngassa ni mmoja kati ya wachezaji aliokuwa akiwaheshimu kwa kiasi kikubwa na kusema kuwa ndiye aliyempa changamoto ya kujituma na kufika alipo sasa.
“Namheshimu sana Ngassa na ni yeye aliyekuwa akinifanya nijitume kila siku ili nimfikie, vitu vingi nilikuwa namuiga yeye sasa ukiniambia kuvaaa vitu vyake kwa sasa nitakuwa nasema uongo.
“Najua wengi wanadhani naweza kufanya vizuri kumpita Ngassa, lakini ukweli ni kwamba napaswa kujituma zaidi katika mazoezi ili nifikie kiwango chake (Ngassa).”Kaseke amejiunga na Yanga baada ya kumaliza mkataba wake na Mbeya City.

Note: Only a member of this blog may post a comment.