Martha Mboma, Dar es Salaam.
DUH! Kweli noma, kwani Mtibwa Sugar imesema inaweza kuwarudisha nyota wake wote walioondoka na kwenda kuchezea klabu nyingine isipokuwa kiungo mkongwe Shaaban Kisiga tu.
Mtibwa yenye maskani yake Manungu, Turiani mjini Morogoro, imekubali kuwapokea nyota wake hao ambao hawakufanya vizuri msimu uliopita katika klabu nyingine lakini imesisitiza haimtaki tena Kisiga aliyejiengua Simba.
Kuna taarifa kuwa huenda wachezaji Hussein Javu, Nizar Khalfan (waliopo Yanga), Hussein Sharif ‘Casillas’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ wa Simba wakatupiwa virago katika klabu hizo na kurejea Mtibwa. Ofisa Habari wa Mtibwa, Thobias Kifaru, amesema: “Tutawarejesha wachezaji wetu wote walioondoka kama wanataka kurudi lakini siyo Kisiga.”
“Huyu Kisiga hatuwezi kumpokea kwani ana makosa ya mara kwa mara na ni msumbufu, ndiyo maana hata Simba hakuweza kudumu, unadhani akirudi hapa atafanya kitu kipi kama siyo kutusumbua tu?”

Note: Only a member of this blog may post a comment.