Imelda mtema
Mtangazaji mahiri wa Kipindi cha
The Mboni Show kinachorushwa kupitia Televisheni ya Taifa ya TBC1, Mboni
Masimba, amejikuta akiangua kilio kwenye Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili jijini Dar, alipotembelea wodi ya wazazi na kusimulia jinsi
ambavyo daktari alimweleza kuwa ilikuwa kiduchu tu afe wakati wa
kujifungua hivi karibuni.
“Daktari alinieleza kuwa mimi nilikuwa ni wa kufa jamani hapa ndipo niliporejeshewa uhai wangu tena japokuwa nilijifungulia hospitali nyingine lakini huko kote walishindwa, hapa ndipo walinitibu pekee na niliweka ahadi kuwa nitarudi kwa ajili ya kutoa kwa wengine,” alisema Mboni.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Uzazi, Dk. Mathew Kalianga alisema kuwa ugonjwa uliompata Mboni kitaalam unaitwa Pulmonary Embolism ambapo mara nyingi watu wanaopata ugonjwa huo ni asilimia tano tu kati ya mia ndiyo wanapona hivyo Mboni ni mmoja aliyebahatika.
Pulmonary Embolism ni ugonjwa wa Kuganda kwa damu ambao husababisha mshipa mkubwa unaosafirisha damu na hewa kwenda kwenye mapafu kuziba. Hali hiyo huweza kusababisha mtu kufariki dunia ghafla. Ndiyo uliomuua mwanamuziki wa Nigeria marehemu Goldie.
Mboni aliyesindikizwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alitoa msaada wa mashuka, viti vya matairi na vingine vingi vinavyohitajika wodini hapo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.