Issa mnally
AMA kweli duniani
kuna mambo! Mdada anayehangaika kutafuta jina katika tasnia ya muziki wa
Kibongo, Isabella Mpanda ‘Bella’ aliitia doa sherehe yake ya kuvishwa
pete ya uchumba baada ya kunaswa akidendeka na mchepuko dakika chache
kabla ya tukio hilo muhimu.
Paparazi wetu ambaye alikuwepo ukumbini hapo aliwanasa wawili hao katika kona moja yenye giza wakiwa ‘mahaba niu’e huku Inspector akionekana kuwa na wasiwasi wa kuonwa na mwenye mali.
Baada ya kushtushwa na mwanga wa kamera, wawili hao walionekana kuweweseka kwanza kisha, Inspector akaanza kumwomba paparazi wetu kuzifuta picha hizo akidai zikionekana zinaweza kumletea matatizo.
“Kaka soo bwana… soo kaka! Huyu ni shemeji yangu, hapa tuna hang’ tu… noma mkubwa. Hizo picha zikionwa nitafikiriwa vibaya na ‘mwanangu’ (Kalama),” alisema Inspector kwa sauti ya unyenyekevu. Bella yeye alisema: “Halafu hawa kwa kufuatafuata watu hawajambo. Futa bwana hizo picha.”
Note: Only a member of this blog may post a comment.