Na Said AllyDar es Salaam
KIUNGO wa kimataifa wa Yanga, Mbrazili, Andrey Coutinho, amesema hajui kama atarejea Bongo kutokana na uongozi wa klabu yake kutomuambia chochote hadi sasa.
Coutinho, ingawa amebakiza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia Yanga, wakati akiondoka kuelekea Brazil baada ya ligi kumalizika, alisikia tetesi kwamba yeye ni mmoja wa wachezaji watakaotemwa klabuni hapo.
Fundi huyo wa mipira ya adhabu, amesema bado hajui hatima yake, hasa baada ya kuona uongozi haujamwambia chochote tangu anaondoka hadi sasa.
“Kwa sasa nipo likizo baada ya purukushani za kipindi kirefu za michezo ya ligi na ile mingine ambapo licha ya mapumziko hayo, nimekuwa nikijinoa mwenyewe kwa mazoezi binafsi ili kuhakikisha naendelea kuwa bora kwa msimu unaokuja.
“Ila mpaka sasa bado nipo njia panda kuhusiana na lini nitarejea Tanzania na kuungana na klabu yangu kwa kuwa hakuna kiongozi yeyote aliyenipigia hata kuniambia kwamba natakiwa kuripoti lini kambini,” alisema Coutinho.

Note: Only a member of this blog may post a comment.