Hans Mloli na Sweetbert Lukonge
ISHU ya usajili wa mshambuliaji wa zamani wa Simba, Haruna Chanongo kutua Yanga, imechukua sura mpya baada ya juzi staa huyo kukaa mezani na uongozi wa Yanga lakini hakuna kilichokamilika mpaka jana jioni.
Chanongo ambaye amemaliza msimu ulioisha hivi karibuni akiwa na Stand United akiitumikia kwa mkopo kutoka Simba, amekuwa akihusishwa kuwaniwa na timu mbalimbali za Ligi Kuu Bara zikiwemo Stand, Mwadui na Yanga.
Awali, alipotafutwa Chanongo kuhusiana na taarifa hizo, ilikuwa tofauti kwa kuwa alikiri amesaini mkataba na Yanga na wala hakuwa tayari kutoa maelezo ya kina kwamba amesaini wa muda gani kabla ya kukata simu yake ya mkononi.
Lakini wakala wa Chanongo, Jamal Kasongo, amezungumza na Championi Jumatatu na kueleza kuwa kweli walikuwa na mpango wa kumalizana na Yanga juzi Jumamosi lakini hawakuafikiana chochote ingawa bado kuna mawasiliano yanaendelea kati yao.
“Chanongo yeye alikutana na Yanga jana (juzi) akaongea nao baadhi ya mambo tuliyohitaji kuafikiana lakini kwa bahati mbaya hatukupata muafaka kwa kuwa Chanongo alitaka kuwepo na uongozi unaomsimamia masuala yake ya soka katika kikao hicho.
“Kwa hiyo ikaishia hapo lakini Chanongo yeye hana tatizo kuhusiana na hilo, yeye anawasikiliza Yanga kama watakuwa tayari basi atafanya nao kazi,” alisema Kasongo ambaye pia ni wakala wa Mtanzania, Mbwana Samatta anayekipiga TP Mazembe ya DR Congo.
Pamoja na hayo, pia taarifa za uhakika kutoka kwa mtu makini ndani ya Yanga zilifafanua kuwa, uongozi wa timu hiyo mpaka sasa umemalizana na Deus Kaseke wa Mbeya City pekee ingawa wanaweza kumnasa Chanongo lakini itategemea na majaliwa ya hapo baadaye.

Note: Only a member of this blog may post a comment.