MAOFISA saba wa Shirikisho la Soka duniani (FIFA) wamekamatwa na askari kanzu asubuhi ya leo katika hoteli moja mjini Zurich, nchini Switzerland, kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Watuhuhumiwa hao ambao wanasemekana kuwa ni pamoja na Makamu wa Rais wa FIFA, wanashikiliwa wakisubiri kusafirishwa kwenda Marekani.
Shutuma hizo zinahusisha rushwa ya takriban kiasi cha dola za Marekani milioni 100 kwa kipindi cha zaidi ya miaka 20 tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990 kwa ajili ya michuano ya Amerika ya Kati.
Wanachama wa FIFA wanakutana mjini Zurich kwa ajili ya mkutano wao wa mwaka siku ya Ijumaa, ambapo rais wa shirikisho hilo, Sepp Blatter, anawania kiti hicho muhula wa tano.
Mwana wa mfalme Ali Bin Al-Hussein wa Jordan, ambaye ndiye mpinzani pekee wa Blatter amesema tukio hilo ni baya kwa maendeleo ya soka duniani.
Gazeti la New York Times limesema askari kanzu walichukua funguo za chumba cha hoteli kutoka eneo la mapokezi ya hoteli ya Baur au Lac Hotel ambayo maofisa hao walikuwa wakiishi na kuingia vyumbani mwao. Gazeti hilo limesema oparesheni hiyo ilifanyika kwa utulivu.
Jeffrey Webb, Mkuu wa Shirikisho la Amerika ya Kaskazini na Kati na Visiwa vya Caribbean, ametajwa kuwa mmoja kati ya maofisa waliokamatwa.
Maofisa wengine wa FIFA walioshuhudiwa na BBC wakisindikizwa na polisi kutoka kwenye hoteli hiyo ni:
Mkuu wa Shirikisho la soka la Costa Rica, Erduado Li, ambaye alikuwa akitarajia kuwepo kwenye mkutano wa kamati ya FIFA siku ya ijumaa. Wengine ni rais wa shirikisho la Uruguay, Eugenio Figueredo, rais wa shirikisho la soka Amerika Kusini na wa Brazil, Jose Maria Marin na mwanakamati ndani ya FIFA ambaye polisi walionekana wamebeba mikoba yake kwenye mifuko ya Plastiki.
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni kwa vipi Blatter amekuwa kiongozi wa FIFA kwa muda mrefu, pamoja na kuwepo kwa ripoti nyingi za vitendo vya rushwa.
Mwanzoni mwa mwezi huu, Blatter alisema anafahamu baadhi ya wafanyakazi wenzake wa zamani walikuwa wakichunguzwa lakini amekanusha kuwa uchunguzi huo ulimhusu pia.Orodha ya Maofisa waliokamatwa mpaka sasa ni:

- Jeffrey Webb - Makamu wa rais wa FIFA na Mjumbe wa Kamati kuu kutoka Visiwa vya Caribbean.
- Eugenio Figueredo - Makamu wa rais wa FIFA na mjumbe wa Kamati Kuu wa nchini Uruguay.
- Eduardo Li - Mjumbe wa kamati kuu ya FIFA wa kuchaguliwa pia ni rais wa Shirikisho la Soka nchini Costa Rica.
- Julio Rocha – Ofisa Maendeleo wa FIFA na rais wa Shirikisho la Soka nchini Nicaragua.
- Costas Takkas – Mwakilishi wa Rais wa CONCACAF.
- Rafael Esquivel - Mjumbe wa kamati kuu ya CONMEBOL na rais wa Shirikisho la Soka nchini Venezuela.
- Jose Maria Marin – Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka nchini Brazilian.
CHANZO: DAILY MAIL NA BBC
Note: Only a member of this blog may post a comment.