Wednesday, April 8, 2015

Anonymous

VIDEO: INASIKITISHA SANA! Tazama Polisi wa kizungu akimpiga risasi na kumuua mtu mweusi!

Polisi wa kizungu wa South Carolina nchini Marekani, jana Jumanne alishtakiwa kwa kosa la mauaji, saa chache baada ya maofisa kutazama video ya kushangaza inayomuonesha akimpiga risasi mgongoni na kumuua mwanaume mwenye asili ya Afrika aliyekuwa akikimbia. 

Meya wa North Charleston, Keith Summey alitangaza mashtaka hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari ambapo alisema polisi huyo aitwaye Michael Thomas Slager alichukua uamuzi mbaya. Aliyeuawa anaitwa Walter Lamer Scott mwenye umri wa miaka 50.
Video hiyo iliyosambazwa kwenye vituo vya runinga inamuonesha ofisa hiyo akimmiminia risasi mgongoni mtu huyo wakati akikimbia.
Mtu aliyechukua video hiyo hajulikani.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.