Rais Kikwete alikuwa akiongea wiki hii nchini Marekani kwenye kituo cha kimataifa cha wasomi cha Woodrow Wilson kilichopo jijini Washington DC.
“Baada ya miaka 10, unahitaji kuendelea na maisha mengine. Imekuwa ni miaka 10 tangu niingie kwenye majukumu haya makubwa,” alisema.
“Nilikuwa mdogo, miaka 55 tu. Lakini kile ninachoweza kuwaambia kuhusu kazi hii ni kwamba ina stress na haina shukrani,” aliongeza.
Alipoulizwa kwanini marais wengine wa Afrika hupenda kung’aninia madaraka, Kikwete alijibu: Siwezi kuzungumza kwa niaba yao. Inabidi muwaalike ili mpate mawazo yao.”
-via bongo5

Note: Only a member of this blog may post a comment.