Monday, April 6, 2015

Anonymous

Unadhani tatizo la ajira liko Bongo peke yake? Lazima Ukae Ukiisoma hii ya Jamaa huyu wa Uingereza

Mtaa anaoishi Huw Davies
Tatizo la ajira ni kilio cha vijana wengi TZ, watu wanalalamika kwamba wamesoma lakini hawajaajiriwa.. unadhani hili liko BONGO peke ake?

Jamaa mmoja Uingereza, Huw Davies ana degree ambayo ameipata mwaka 2002 baada ya kusoma Chuo cha Glamorgan, lakini toka amemaliza mpaka leo hii amekuwa anatafuta kazi.. ni kwamba hajaajiriwa mpaka leo.

Huw Davies
Jamaa huyo mwenye degree ya Geography amekuwa akitafuta kazi inayoendana na taaluma yake ya masuala ya mazingira kwa miaka 13, ambapo mpaka sasa ameshaomba kazi mara 500, lakini hajawahi kuitwa kwenye Interview hata mara moja

Davies hajataka kufanya kazi nje ya Uingereza, bado ana imani kwamba atapata kazi tu siku yoyote.. kwa sasa anasema yuko tayari kufanya kazi yoyote hata ya kuendesha taxi.
-via millardayo

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.