Akizungumza kwa njia ya simu jana, Tahliya alisema: “Namwachia Mungu suala hili, siwezi kuchukua hatua zaidi ya hapa.”
Ummul Khayr Sadir Abdulla, alikamatwa Machi 30
katika mpaka wa Kenya na Somalia, El Wak, Jimbo la Mandera kwa kile
kilichodaiwa kutaka kuingia nchini Somalia ili kujiunga na kundi la
kigaidi la Al-Shabaab.
Bibi na babu wa binti huyo, Masoud Salim na Asha Saleh ambao wote ni walimu walisema hawakufikiria kama jambo hilo lingetokea katika familia yao na kuongeza kuwa wanaamini ni suala la utoto tu.
Bibi na babu wa binti huyo, Masoud Salim na Asha Saleh ambao wote ni walimu walisema hawakufikiria kama jambo hilo lingetokea katika familia yao na kuongeza kuwa wanaamini ni suala la utoto tu.
“Sisi hii taarifa tumeipata kupitia vyombo vya habari” aliongea bibi huyo akitokwa machozi.
Bibi huyo alisema familia nzima ina wasiwasi mkubwa kutokana na ukubwa wa shutuma hiyo inayomkabili mjukuu wao na hawajui mwisho wake.
Bibi huyo alisema familia nzima ina wasiwasi mkubwa kutokana na ukubwa wa shutuma hiyo inayomkabili mjukuu wao na hawajui mwisho wake.
Naye, Masoud Salim alisema anaamini kuwa mjukuu
wake anajua anachokifanya kwani mara ya mwisho, aliwaaga anakwenda
masomoni Sudan ambako yeye na dada yake Sumaiya wanasomea fani ya
udaktari.
Salim alisema baba na mama yake Ummul- Khayr wako nchini Kenya kufuatilia suala hilo.
Salim alisema baba na mama yake Ummul- Khayr wako nchini Kenya kufuatilia suala hilo.
Hata hivyo, Mwananchi lilipozungumza na mama yake Ummul Khayr, Tahliya alikataa kusema yupo wapi kwa wakati huo.
Ummul-Khayr ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Kimataifa cha Afrika, Sudan alikamatwa nchini Kenya akiwa na wenzake
wawili raia wa Kenya, Maryam Said Aboud na Khadija Abubakar Abdulkadir.
Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, DCI Diwani Athuman alisema bado wanasubiri majibu kutoka kwa polisi wa Kenya ili kuendelea na taratibu za kumrudisha msichana huyo nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, DCI Diwani Athuman alisema bado wanasubiri majibu kutoka kwa polisi wa Kenya ili kuendelea na taratibu za kumrudisha msichana huyo nchini.
“Tumeshangaa hatujajibiwa lolote mpaka sasa, lakini wakitujibu taratibu zote zitafuatwa,” alisema DCI Diwani
Ummul-Khayr alimaliza madarasa ya Quran Zanzibar na baadaye alipata elimu yake ya juu katika Shule ya SOS kabla ya kujiunga na elimu ya Chuo Kikuu nchini Sudan.
Ummul-Khayr alimaliza madarasa ya Quran Zanzibar na baadaye alipata elimu yake ya juu katika Shule ya SOS kabla ya kujiunga na elimu ya Chuo Kikuu nchini Sudan.
Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abbas Irovya alisema, ofisi yake imehakiki uraia wa msichana huyo na kujiridhisha kuwa ni Mtanzania.
-MWANANCHI
-MWANANCHI

Note: Only a member of this blog may post a comment.