Wednesday, April 22, 2015

Anonymous

Taarifa nyingine kuhusu uchaguzi mkuu 2015 na uporaji Dar, Moshi...Bajeti ya mwisho ya JK #PBCloudsFM

elections_afrique_3
Nimekusogezea stori kubwa mtu wangu zilizosikika kwenye Magazeti ya leo April 22, ipo ya bajeti ya mwisho kwa Serikali ya awamu ya nne inayotarajiwa kujadiliwa April 27, NEC imesema kuna uwezekano kura ya maoni ikafanyika pamoja na uchaguzi mkuu October 2015,  Dr.Slaa amesema wamegundua NEC imeanza kuandikisha wapiga kura kwenye mikoa ambayo ni ngome ya CCM, imesikika na hii ya mlinzi wa Askofu Gwajima kajisalimisha Mahakama ya Kisutu. 

Nyingine iliyosikika ni ishu ya raia 12 wa Iran na Pakistan wanaokabiliwa na kesi ya kuingiza mihadarati nchini kuelezea kuchoshwa na kesi yao kuchukua muda mrefu, ipo ya tukio la Polisi Dar kuwakamata watuhumiwa wanne waliojihusisha na tukio la uporaji, kutoka Moshi gari la kiwanda cha Bonite limevamiwa na wafanyakazi wawili kuuawa, madereva wa mabasi na malori wameelezea kusikitishwa na Serikali kwa kushindwa kufanya mazungumzo na Serikali imeendelea kutekeleza mikakati ya kutoa wataalamu wengi wa Sayansi.
Hii imesikika kwenye PowerBreakfast @CloudsFM, bonyeza play…

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.