Sweetbert Lukonge Dar es Salaam
UONGOZI wa Simba unahangaika huku na kule kuhakikisha unakiimarisha kikosi chake kwa ajili ya michuano ya Ligi Kuu Bara msimu ujao baada ya msimu huu kuonekana kutokuwa imara.
Katika kufanikisha mpango huo, baadhi ya wajumbe wa kamati ya usajili ya klabu hiyo hivi karibuni walivamia mkoani Morogoro na kufanya mazungumzo na nyota wa Yanga ambaye sasa anaitumikia Polisi Moro kwa mkopo, Said Bahanuzi.Simba ina mpango wa kutaka kumsajili Bahanuzi ili aweze kuiongezea nguvu safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ambayo msimu huu haijaonyesha makali yake kama ilivyozoeleka.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba zimedai kuwa, viongozi hao ambao wapo katika kamati ya usajili ya timu hiyo, walifunga safari mpaka Morogoro mwishoni mwa wiki iliyopita, kwa ajili ya mazungumzo na Bahanuzi. “Bahanuzi muda wowote anaweza kuingia mkataba na sisi baada ya mazungumzo naye juu ya kumsajili kwenda vizuri.
“Wiki iliyopita tulifanya naye mazungumzo mkoani Morogoro na tumefikia sehemu nzuri sasa ila jibu kamili kuhusiana na mpango huo utalipata baada ya Sikukuu ya Pasaka,” kilisema chanzo hicho cha habari.
Bahanuzi alipotafutwa ili azungumzie suala hilo, hakuweza kupatikana baada ya simu yake ya mkononi kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
Hata hivyo, Championi Jumatatu lilienda mbali zaidi na kuzungumza na mmoja wa viongozi wa Benchi la Ufundi la Polisi Moro ili kujua kama ni kweli Simba wameshazungumza na Bahanuzi.Bila ya kuficha kiongozi huyo alisema: “Tafadhali naomba usitaje kama mimi ndiye nimekwambia suala hili, ukweli ni kwamba wiki iliyopita viongozi watatu wa Simba walikuja Morogoro na wamezungumza naye na jinsi inavyoonekana anaweza akajiunga na timu hiyo.
“Hata hivyo, jana (juzi Jumamosi) nilizungumza na Bahanuzi akaniambia kuwa kinachoweza kukwamisha mpango huo ni mkataba wake na Yanga lakini yeye yupo tayari kutua Simba na hapendi kuendelea kuwa na Yanga,” alisema kiongozi huyo.
Bahanuzi ambaye alisajiliwa na Yanga mwaka 2012 akitokea Mtibwa Sugar bado anamkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo ambayo kwa sasa inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Note: Only a member of this blog may post a comment.