Shamsa Ford wa Nay wa Mitego ndani ya Burundi!
Mwanadada anayefanya vizuri kwenye filamu nchini Shamsha Ford a.k.a mama Ney wa mitego ameendelea
kuiwakilisha vyema tasnia ya filamu nchini baada ya kualikwa nchini
Burundi na wasanii wakubwa wa filamu nchini humo kwa ajili ya kufanya
filamu pamoja nao.
Shamsa amesema kuwa filamu hiyo itawahusisha wasanii tofauti
kutoka Rwanda,Burundi,Uganda Tanzania, na amewaomba watanzania wamuombee
heri ili afanye vizuri kwenye filamu hiyo.
Hapo jana mwanadada Shamsa alipata nafasi ya kuongea na
waandishi wa habari juu ya filamu hiyo mpya ambayo bado terehe ya kutoka
kwake haijajulikana.
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Note: Only a member of this blog may post a comment.