Monday, April 20, 2015

Anonymous

SAD NEWS: WATU 18 WAFARIKI CHANZO IKISEMEKANA NI DAWA YA MAGUGU!

Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema inavyoelekea dawa ya kuuwa magugu ndio chanzo cha vifo vya watu 18 vilivyotokea kusini-magharibi mwa Nigeria, bila ya sababu kujulikana.

Katika siku chache zilizopita wakaazi katika jimbo la Ondo wamekufa saa chache baada ya kuhisi macho hayaoni sawasawa na kuumwa na vichwa baadae wanazimia.

Msemaji wa WHO alieleza kuwa ukaguzi uliofanywa hadi sasa kutafuta virusi au bacteria haukugundua kitu.
Alisema kwa sasa mawazo yao ni kuwa vifo hivyo vilisa-babishwa na dawa ya kuuwa magugu.
-BBC

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.