Sunday, April 19, 2015

Anonymous

Ray C Afunguka Tetesi za Kujisogeza Tena Kwa Lord Eyez Aliyemfundisha Kutumia Unga!

Ngoma mpya itakayotoka hivi karibuni ambayo Lord Eyez amemshirikisha Ray C haimaanishi kuwa mastaa hao waliowahi kuwa wapenzi wamerudisha ukaribu wao.
Kwa mujibu wa Ray C, wimbo huo ulirekodiwa miaka 7 iliyopita.

Ray C amepost picha hii kwenye Instagram na kuitolea maelezo hapo chini...
“Mambo iende kwa wote wanipendao!Naomba tu kuwajulisha kuwa Nimeskia Lord Eyes anakaribia kuutoa wimbo uitwao Matatizo ambao alinishirikisha!Najua wengi wanaweza tafsiri vingine lakini Niwambie tu kwamba Huu wimbo tuliurekodi miaka SABA ILiopita nchini Kenya kipindi tuko pamoja na si kipindi cha hivi karibuni!Nimeona niongee tu maana naona magazeti yashaanza Udaku,” ameandika Ray C kwenye Instagram.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.