Thursday, April 30, 2015

Anonymous

Mwalimu kaona bora afanye biashara ya kuuza nguo kuliko hii ya kufundisha, kisa nini?!

Dump
Kaskazini mwa Kenya hali sio shwari.. mara nyingi yameripotiwa matukio ya ugaidi, nakumbuka kuna tukio la basi kutekwa watu wakauawa.. likatokea tukio jingine la wanafunzi zaidi ya 140 kuuawa katika shambulio la Chuo Kikuu Garissa.

Hii stori imeripotiwa leo na kituo cha TV cha K24.. mwalimu huyu alishuhudia lile tukio la basi kutekwa, wenzake waliuawa huku akishuhudia.. hataki kurudi tena kufundisha, kaamua kuanza biashara ya kuuza nguo za mitumba. 

Japo analalamika kwamba kwa sasa hali sio nzuri, kipato ni kidogo sana kwa sababu Serikali haimlipi tena mshahara wake lakini hana jinsi, hawezi kurudi kufundisha sehemu ambayo haina usalama.
Unaweza kuisikiliza  hapa stori niliyokurekodia kwenye kituo cha K24

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.