Thursday, April 30, 2015

Anonymous

BALAA TUPU! Kutana na Wanawake Hawa Hatari Sana Jijini Dar. #Hekaheka

gea
Matukio ya wanawake kuiba kwenye maduka ya nguo yanatokea sana Dar hasa maeneo ya Kariakoo.. kuna dada mmoja aliwahi kukamatwa akapigwa na kuvuliwa nguo..Hekaheka ya leo inahusu wasichana watatu walioenda kuiba nguo kwenye duka moja maeneo ya Magomeni Morocco. 

Dada muuza duka amesema alikuwa anawahudumia wateja wengine wakaingia wadada watatu waliovaa majuba na nikabu.. baadae akaambiwa na mtu kwamba wanawake hao wameiba nguo wakati yeye akihudumia wateja wengine.. watu wakawakamata lakini mmoja wao alikimbia ambaye mashuhuda wanasema kuwa ndiye aliyeiba nguo hizo. 

Wanawake hao walisema walikua wametoka msikitini, wakapitia dukani hapo lakini hawahusiki na wizi huo. Baadae waliwapigia simu ndugu zao wakaja wakaomba ndugu zao waachiwe na wao walikuwa tayari kulipa gharama ya nguo ambazo zimeibiwa na mmoja wa wanawake hao ambae alikimbia. 

Wanawake hao wamesema hawakuwa wanafahamiana na huyo mwanamke aliyekimbia na nguo alizoiba hapo kwenye duka.. wanasema wao walimkuta mwanamke huyo dukani kama ambavyo walikuta wateja wengine.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.