Serikali imesema inafuatilia kwa karibu
maelezo yanayotolewa na Mtanzania Rashid Mberesero (20) aliyekamatwa
Kenya akidaiwa kufanya ugaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa
uliosababisha vifo vya watu 148.
Aidha, Serikali imewatoa hofu Watanzania na kuwaambia kuwa nchi iko salama katika suala la ugaidi. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe jijini Dar es Salaam jana alipozungumzia mustakabali wa nchi kuelekea kura ya maoni kuhusu Katiba Inayopendekezwa na Uchaguzi Mkuu.
Chikawe alisema wizara yake inafuatilia kwa makini kile anachozungumza Mtanzania huyo katika mahojiano nchini Kenya ili kuweza kubaini kama kuna Watanzania wanaoshirikiana naye.

“Kwa sasa amefikishwa mahakamani, lakini
kama serikali tunafuatilia kila anachokizungumza kwenye mahojiano na
wenzetu wa Kenya ili kuweza kuwabaini kama kuna Watanzania wanaohusika
ambao wapo nchini,” alisema.
Mtanzania huyo anadaiwa kukamatwa baada ya kujificha kwa saa nane akiwa amejichanganya na maiti, lakini baadaye alipanda na kujificha darini akiwa na mabomu.
Mtanzania huyo anadaiwa kukamatwa baada ya kujificha kwa saa nane akiwa amejichanganya na maiti, lakini baadaye alipanda na kujificha darini akiwa na mabomu.
Chikawe alisema tatizo la ugadi ni la kidunia, lakini aliwataarifu Watanzania kuwa nchi iko salama. “Ugaidi ni tatizo la kidunia, sehemu nyingi kuna matatizo kama hayo, napenda niwaambie Watanzania nchi yenu iko salama, tuko salama,” alisema.
Aidha, Chikawe alisema Serikali
itachukua hatua kali kwa watu binafsi, vyama vya siasa na taasisi za
dini zitakazobainika kuvuruga usalama na utulivu wa nchi.
Alisema uzoefu unaonesha kila ifikapo wakati wa kuelekea kufanya chaguzi mbalimbali kumekuwa kukitokea matukio yanayoashiria uvunjifu wa usalama na utulivu.
Alisema uzoefu unaonesha kila ifikapo wakati wa kuelekea kufanya chaguzi mbalimbali kumekuwa kukitokea matukio yanayoashiria uvunjifu wa usalama na utulivu.
Alisema ili kukabiliana na hali hiyo, ni vyema wananchi, vikundi zikiwemo taasisi za dini kuepuka kushiriki katika vitendo vinavyoashiria kuvuruga amani na utulivu na kuwa serikali itachukua hatua za kisheria kudhibiti hali hiyo.
“Kazi ya serikali ni kuhakikisha kuwa
usalama wa watu wote unaimarishwa ili shughuli zote zikiwa ni za
kisiasa, kidini, kijamii na kiuchumi zinatekelezwa kwa misingi ya
kisheria,” alisema.
Chikawe ameonya viongozi wa taasisi za dini kutoendelea kutoa matamko yanayoashiria kuingilia masuala ya kisiasa kinyume na sheria ya vyama na katiba zinazosimamia uendeshaji wa taasisi hizo.
Chikawe ameonya viongozi wa taasisi za dini kutoendelea kutoa matamko yanayoashiria kuingilia masuala ya kisiasa kinyume na sheria ya vyama na katiba zinazosimamia uendeshaji wa taasisi hizo.
Alitolea mfano tamko lililotolewa na viongozi wa taasisi za dini wakilenga kuwashawishi waumini wao wafuate maelekezo yao kuhusiana na masuala ya Katiba Inayopendekezwa na kuhusu uchaguzi mkuu ujao.
Alisema viongozi wa taasisi za dini wana haki ya kushiriki katika masuala ya kisiasa kama watu binafsi ila ni kinyume cha sheria kutumia uongozi wao kushawishi waumini wao watekeleze matakwa yao ya kisiasa.
“Mfano mwingine ni pale kiongozi au
viongozi wa dini wanapochangisha fedha na kuandamana au kukutana na
wanasiasa kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kuwashawishi kugombea nafasi
mbalimbali za uongozi. Hii si kazi ya taasisi za dini na ni kinyume cha
sheria,” alisisitiza.
-HABARILEO

Note: Only a member of this blog may post a comment.