Naibu Waziri wa Sayansi, Teknolojia na
Mawasiliano, Januari Makamba pichani juu ametajwa kuwa mwanasiasa bora kijana na
taasisi ya Tanzania Awards International, jijini Dar es Salaam juzi.
Makamba ameshika nafasi hiyo akiwapita
wanasiasa wengine vijana ambao ni pamoja na Kiongozi wa chama cha ACT
Wazalendo, Zitto Kabwe, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye,
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, Naibu Waziri wa Fedha
Mwigulu Nchemba, Wabunge Vick Kamata, Esther Bulaya, David Kafulila na
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Mboni Mhita.
Katika tuzo za mwanasiasa mtu mzima ushindi umechukuliwa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na katika kundi hilo, Profesa Muhongo alishindanishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, Waziri Sheria na Katiba, Dk. Asha Rose Migiro na Waziri wa Nchi Katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano, Samia Suluhu.
Wengine ni Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Liberata Mulamula.
Tuzo ya jamii ilichukuliwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi.
Waliopewa tuzo za heshima katika jamii ni Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere na Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela.
Si Makamba, Profesa Muhongo wala Mengi waliohudhuria shughuli hiyo badala yake waliwakilishwa na ndugu zao.

Hata hivyo sherehe za kutoa tuzo hizo
zilidororora hasa kwa kuwa Rais Jakaya Kikwete aliyepangwa kuwa mgeni
rasmi hakuhudhuria na aliwakilishwa na mkuu wa mkoa lakini naye
aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Akitoa ufafanuzi wa tuzo hizo, Mratibu wa Taasisi hiyo, Amani Mwaipaja alisema zilikuwa katika vipengele vitano ambavyo ni tuzo ya jamii 2015, tuzo za jamii ya heshima, tuzo jamii katika haki za binadamu, tuzo ya mwanasiasa kijana na tuzo ya mwanasiasa mzee.

“Tumeangalia vigezo kadhaa ikiwa pamoja
na uadilidu, uaminifu, utii katika sheria, kuwa na maono, mikakati na
mipango,” alisema Mwaipaja.

Note: Only a member of this blog may post a comment.