Ni
ndege ambayo ilianza safari yake March 9 2015 Abu Dhabi na ikafanikisha
salama safari zake kwa kupaa angani na kupita Oman, India na Myanmar.
Marubani wawili wanaoiendesha wanasema
wanataka kuvunja rekodi kwa kuuthibitishia ulimwengu kwamba Ndege
inayotumia nguvu ya Jua inaweza kutumika kwenye dunia ya sasa.
Pamoja
na hayo, safari yao bado ni ndefu ambapo siku mbili zilizopita
waliripotiwa na CNN kwamba safari yao imekwama China kwa zaidi ya wiki
mbili baada ya kushindwa kupaa kutokana na hali mbaya ya hewa, hali
ikiwa mbaya inavunja masharti ya kuipaisha ndege hii.

Note: Only a member of this blog may post a comment.