Sunday, April 19, 2015

Anonymous

KUMEKUCHA CCM: Hii hapa Kuhusu Mkakati wa kuwatema LOWASSA na MEMBE

Wakati mchakato wa CCM kutafuta mgombea Urais ukitarajiwa kuanza mwezi ujao, imebainika kuwa kuna mkakati wa kuyapiga chini makundi ya makada wanaosaka urais ili kupata mgombea ayakayekinusuru chama  hicho katika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu. 

CCM imekuwa ikipata wakati mgumu kila mwanachama wake anapomaliza vipindi vyake viwili vya urais, na safari hii kazi ya kumpata mrithi wa Rais Jakaya Kikwete ambaye amepata urais mwaka 2005 inaonekana kuwa ngumu zaidi na huenda ikasababisha chama hicho kupunguzwa nguvu zaidi iwapo haitafanya uamuzi unaokubalika na makundi yote  ya Urais. 

Makundi makubwa yanayolengwa na mkakati huo wa kuyapiga panga, ni ya makada wanaoonekana kuwa na nguvu na ushawishi mkubwa ambayo kambi zao zimekuwa zikipambana  vikali kwenye vita ya chini kwa chini ya Urais. 
Makundi hayo ni lile linalomuunga mkono Lowassa na linalomuunga mkono Membe,watu wanauwaunga mkono makada hao wamekuwa wakipishana mikoani kuweka mambo sawa kwa vigogo hao, hali ambayo inaonekana kuwatisha CCM kiasi cha kuchelewa kutangaza kwa mchakato wa Urais ndani ya chama hicho. 

Tayari makada hao na wenzao wamepwa onyo kali inayowazuia kuwania nafasi yoyote kwa kipindi cha miezi 12 na adhabu hiyo ilikuwa imalizike Februari mwaka mwaka huu lakini imeongezwa muda kutokana na kamati ya maadili kuendelea na uchunguzi.
-MWANANCHI

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.