FC Barcelona wakiwa katika uwanja wao wa
nyumbani leo wamefanikiwa kuvuka kwenda hatua ya nusu fainali ya
michuano hiyo baada ya kuifunga PSG kwa magoli 2-0 na hivyo kupata
ushindi wa jumla wa 5-1 ambapo Neymar alifunga magoli yote mawili katika
mchezo huo.
Huko nchini Ujerumani katika uwanja wa
Allianz Arena, FC Bayern wamefanikiwa kuiondoa FC Porto kwenye michuano
hii kwa ushindi wa 6-1.
Magoli ya Bayern yalifungwa na Alcantara,
Boeteng, Lewandoski aliyefunga mawili, Muller na Xabi Alonso akifunga la
6 huku Jackson Martinez akifunga goli moja la Porto ambapo kwa ushindi
huo Bayern anaing’oa nusu fainali akiwa na jumla ya ushindi wa magoli
8-4.
Ligi hii itaendelea leo kwa mechi ya Atletico Madrid vs Real Madrid na mechi nyingine ni Juventus vs Monaco.

Note: Only a member of this blog may post a comment.