Sunday, April 19, 2015

Anonymous

KIMENUKA MBAYA: Watanzania waamua kushika silaha Afrika Kusini


Raia wa kigeni wakiamua kujihami kwa kuchukua silaha kupambana na wenyeji.
Raia wa Tanzania wanaoishi Afrika Kusini sasa wanadaiwa kushika silaha tayari kwa mapambo dhidi ya vikundi vya raia wa Taifa hilo vinavyoshambulia wahamiaji wa Kiafrika. 

Taarifa zilizolifikia Gazeti hilo kutoka kwa Watanzania hao imeeleza  hatua hiyo imefikiwa baada ya kupatikana kwa taarifa zinazodai kuwa wenzao wawili wameuawa katika machafuko ya jiji la Durban ambayo chanzo chake ni mashambulizi yanayofanywa na raia wan chi hiyo dhidi ya wageni. 

Mmoja wa Watanzania anayeishi Cape Town, Pius Mbawala alieleza kuwa  taarifa za mauaji ya wenzao zimewasikitisha sana na kwamba hadi sasa hakuna kiongozi yoyote wa ubalozi wa Tanzania aliyewasiliama nao ili kujua hali za usalama wao tofauti na balozi za nchi nyingine. 

Mbalawa alisema kwa muda mrefu sasa maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini humo wamekuwa na uhusiano wenye shaka na Watanzania walioko huko tofauti na wanavyopaswa kujua ukazi wao kwenye Taifa hilo. 

Alisema Raia wa Tanzania wanaoishi nchini humo wamejiunga katika makundi madogo madogo kulingana na maeneo wanayoishi kwa ajili ya kujilinda wenyewe na kila kundi hivi sasa limejihami kwa silaha.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.