Msanii wa Bongo Fleva H.Baba ambaye wiki iliyopita mke wake Florah
Mvungi alijifungua mtoto wa pili wa kiume, amesema kuwa majina aliyoamua
kuwapa watoto wake ni maamuzi yake mwenyewe ili kuwa tofauti na watu
wengine.
H.Baba na mtoto wake wa kwanza Tanzanite
Mtoto wa kwanza wa kike H.Baba amempa jina Tanzanite, na wa pili aliyezaliwa wiki iliyopita wa kiume amepewa jina la Afrika.
“Siri ya majina haya ni kwamba H.Baba yuko tafauti na watu wengine…kwahiyo hayo majina siri kubwa ni maamuzi ya baba mwenyewe, yaani mimi ndio nimeamua, tokea nasoma yaani nilipanga watoto wangu nitawaita majina haya” H.Baba ameiambia 255 ya Clouds Fm
“Pande zote mbili za familia ni kwamba tunaelewana vizuri…ukoo wa Mvungi na ukoo wa Baba hauna matatizo wote wamekaa wamezungumza hawana neno, na jina huyu Afrika ndo kaishakuwa Afrika na Tanzanite tayari habari ya mjini hakuna anayeitwa Tanzanite tena.”
H.Baba amesisitiza kuwa baada ya kumpata Afrika tayari idadi ya watoto wawili aliowahitaji imetimia hivyo kilichobaki ni kazi tu.
“Ndo tayari nimeshamaliza watoto wangu niliokuwa nawataka, kwahiyo Mwenyezi Mungu amenijalia nimepata mtoto wa kiume saizi nataka tufanye kazi, mama afanye kazi mimi nifanye kazi.”
-via bongo5

Note: Only a member of this blog may post a comment.